▶
PSEAH: Kulinda Heshima na Usalama Kazini
Kulinda heshima na kuhakikisha usalama ni kiini cha kazi yetu katika Heinrich Böll Stiftung (HBS).
Hapa tunaeleza Sera yetu ya PSEAH inayo himiza ulinzi dhidi ya uyanyasaji wa Kijinsia, na ukaliti na kueleza wajibu wetu wa pamoja wa kudumisha mazingira ya kazi yaliyo salama, yenye heshima na uwajibikaji kwa wafanyakazi wa hbs na washirika wote.
HBS inasimamia heshima kamili kwa haki za binadamu na haki ya kijamii kwa wote. Demokrasia ya kijinsia na sera ya kutovumilia kabisa aina yoyote ya uyanyasaji wa kijinsia, ukatili na unyanyasaji vimejikita katika viwango vya kikanuni, kimipango na kiutawala ndani ya taasisi.
Tumejizatiti kulinda misingi hii yote ya msingi na tunaiona kama jukumu la pamoja na wajibu wa kila mfanyakazi, washirika na watu binafsi wanaoshirikiana nasi.
Tunaendeleza msimamo wa kutovumilia kabisa uyanyasaji wa kijinsia, ukatili, ikiwemo ukatili au matumizi mabaya ya mamlaka au cheo kwa madhumuni ya kijinsia, vitendo visivyokubalika vya kujamiiana, na mahusiano ya kingono yanayohusisha kubadilishana na faida za kazi. Vitendo vya kingono vinavyohusisha watoto ni marufuku kabisa, na ukiukaji wowote unachukuliwa kwa uzito mkubwa.
Unaweza ukaripoti kwa usiri kesi zozote za PSEAH kupitia: pseah@ke.boell.org
