▶
UNESCO na Super Sema kushirikiana kuwafunza watoto jinsi ya kuwa ‘Shujaa wa Kidijitali’
account_balance
UNESCO - United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization
business
UNESCO
place
Paris
Ili kusherehekea Wiki ya Kimataifa ya Ufahamu wa Vyombo vya Habari na Taarifa, UNESCO imeshirikaina na Super Sema - shujaa wa Afrika ambaye hutumia sayansi, teknolojia, uhandisi, hisabati na sanaa kuokoa ulimwengu- kuzindua wimbo unaoitwa “Shujaa wa Kidijitali”
Wimbo huu unaowalenga watoto kati ya miaka 4 mpaka 12, utawawezesha kutambua taarifa zenye maudhui ya uwongo, na hata kuwapinga wanyanyasaji wa mtandaoni. Watoto watapata ufahamu na ujuzi unaohitajika ili kuwa werevu, wema na wajasiri mtanadoni. Wimbo unalenga kuwapa msingi bora wa muda wao mtandaoni na vilevile, kujenga tabia nzuri wanopotumia vifaa vya kidijitali kuingia mtandaoni. Watoto watafunzwa:
• Jinsi ya kuhoji wanachokiona matandaoni
• Tofauti kati ya ukweli na maoni
• Jinsi ya kutambua maudhui ya uwongo au ya kupotosha
• Umuhimu wa heshima na fadhili mtandaoni
Ungana na kundi la kimataifa lenya lengo la kukuza watoto kuwa raia wa kidijitali. Bonyeza cheza, imba kwa kufuata wimbo na uwe #ShujaawaKidijitali leo!
#GlobalMILWeek
